Hofu imetanda wilayani Karatu katika Mkoa wa Arusha baada ya tukio la kwanza la uchunaji ngozi kuripotiwa katika mji mdogo wa Karatu
Binti mdogo mwenye umri wa miaka tisa, ameuawa mjini Karatu baada ya kutekwa nyara na watu wasiojulikana wakati akielekea machungani na mifugo
Mtoto huyo, Witness Andrew ambaye alikuwa ni Mwanafunzi wa darasa la kwanza kwenye Shule ya msingi ya Sumawe, alipatikana Jumatano usiku, akiwa tayari amekufa baada ya kuripotiwa kupotea kwa zaidi ya saa 24 tangu alipoondoka nyumbani kwao akiwa anaswaga ng'ombe na mbuzi, Jumanne iliyopita
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kiwandani ambako mwili wa mtoto huyo ulipatikana, Alexander Lulu amesema maiti ya mtoto huyo ilikutwa ikiwa imetupwa shambani na baadhi ya viungo vikiwa vimenyofolewa pamoja na ngozi iliyochunwa na kuondolewa kabisa
Witness pia alikutwa bila mguu, mkono na sehemu zake za siri na baadhi, baadhi ya wakazi wa kijiji cha Tloma wanadai ni masuala ya ushirikina
Mtoto huyo ni wa kwanza kuchunwa ngozi katika eneo la Karatu na tayari hofu imeanza kutanda hapa, watu wakihofia kuwa wanachuna ngozi watakuwa wamevamia wilaya hiyo
Baba wa Marehemu, Andrew Paulo na Mama Paulina Petro wanasema mtoto wao alipotea tangu Jumanne wiki hii alipotoka na mifugo kwenda kuchunga kwenye uwanja wa Tloma, lakini hakurudi nyumbani, na kwamba mifugo aliyokuwa nayo ilirejea yenyewe
"Tulimtafuta mtoto kila mahala, lakini bila mafanikio, hata tulipokuta maiti yake eneo la Kiwandani, tulishangaa maana tulishapita kwenye mashamba hayo mapema, lakini hatukununua."walisema wazazi
Wanakijiji wa Tloma wanaamini kuwa mtoto huyo alitekwa na kupelekwa eneo jingine ambako niko alichinjwa kabla ya wauaji wake kumrudisha na kumtupa Kiwandan
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA