Wapinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanasema mazungumzo ya namna Rais Joseph Kabila (pichani) atakavyoondoka madarakani yanalegalega na yamkini yakasambaratika.
Kwa mujibu wa Félix Tshisekedi mmoja kati ya vinara wa upinzani, pande husika katika mazungumzo hayo zinakaribia kusambaratika kuliko kupata suluhisho.
Jana mazungumzo baina ya serikali na vyama vya upinzani chini ya upatanishi wa Kanisa Katoliki yamefanyika mjini Kinshasa. Jana Alhamisi makasisi wapatanishi walikutana na Rais Kabila pamoja na kiongozi mkongwe wa upinzani Etienne Tshisekedi
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA