Katibu Mkuu TAMISEMI 'amfunga breki' DC Polepole

Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa,Mhandisi Mussa Iyombe amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Humphrey Polepole kuacha utaratibu wa wafanyabiashara wa Soko la Ndizi Mabibo uendelee.


Katibu Mkuu Iyombe ametoa agizo hilo jioni ya leo alipokutana na wawakilishi wa wafanyabiashara wa soko hilo ofisini kwake. Akitoa agizo hilo kupitia kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ubungo,Katibu Mkuu Iyombe ametaka utaratibu wa kukusanya ushuru na ulipaji kodi uliokuwepo uendelee.

Katibu Mkuu Iyombe amesema kuwa kama kutakuwa na haja ya mabadiliko au maboresho yoyote,wafanyabiashara wahusishwe. DC Polepole 'alilichukua kimabavu' soko la Mabibo na kuanza kukusanya mapato sokoni hapo kupitia watumishi wa Halmashauri bila kujali uwepo wa Kampuni ya Majimoto ya wafanyabiashara hao iliyopangishwa eneo hilo na Kiwanda cha Urafiki,mmiliki wa eneo husika.

Chapisha Maoni

0 Maoni