DAR ES SALAAM: Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amepiga marufuku kampuni zinazohusika na suala la kukusanya ushuru wa maegesho ya magari katikati ya Jiji la Dar es Salaam, kuacha kufunga minyororo kwenye magari ambayo yanaengeshwa ndani ya muda mfupi, na kuagiza kuwa wanapaswa kusubiri mpaka saa moja ipite, endapo mwenye gari atakuwa hajatokea ndiyo waendelee na taratibu nyingine.
Pia Meya Mwita amewataka wafanyakazi wa kampuni hizo, kuhakikisha muda wote wanavaa sare ili iwe rahisi kuwatambua.Ameongeza kuwa hadi sasa, tayari zimepatikana zaidi ya mashine 850 ambazo kuanzia Januari, 2017 zitaanza kutumika kukusanyia ushuru wa maegesho ya magari, tofauti na sasa ambapo risiti za kawaida zinatumika.
Amesema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha wanadhibiti mapato yanayopatikana kutokana na maegesho ya magari, ili fedha hizo ziweze kutumika kwa shughuli nyingine na kuboresha miundombinu.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA