

MKUU wa Mkoa Wa Mbeya Amos Makalla leo ametembelea soko la ndizi la Kiwira na kufanya mkutano wa hadhara na kueleza Azma YA serikali YA Mkoa wa Mbwya kuliboresha soko la ndizi la kiwira kuwa soko la kimataifa kwani mpska SASA ni wafanyabiashara wengi toka nchi za jirani wanalitumia soko hilo

Kuboresha kwa soko Hilo kutaongeza biashara na litarasimisha biashara na kuongeza mapato kwa wafanyabiadhara na serikali

Aidha amekabidhi Fedha taslimu shilingi milioni MBIILI ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa mwezi uliopita kwenye harambee YA kuchangia mradi wa Maji Kijiji cha Ilundo kata YA Kiwira

Amekemea tabia YA baadhi YA wanasiasa kuendekeza malumbano YA kisiasa na kukwamisha shughuli za maendeleo na amewataka kwa pamoja washirikiane kukabiliana na changamoto YA ujenzi wa vyoo na madarasa katika Shule za msingi na sekondari
Amesema maendeleo yasichanganywe na itikadi YA vyama vya Siasa sasa hivi wananchi washiriki shughuli za maendeleo na Siasa ni mwaka 2019 kwenye uchaguzi wa serikali za vitongoji,Vijiji na mitaa na uchaguzi Mkuu 2020

Hivyo kwa sasa kama kiongozi wa Kijiji, Diwani au mbunge wananchi wampe ushirikiano bila kujali katoka Chama Gani

0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA