Mrisho Ngassa: Najua kuna maneno na minong'ono mingi kuhusu uwezo wangu, muda si punde yataisha.

Hatimaye mchezaji Mrisho Ngassa aliyekuwa anacheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Fanja Fc ya Oman, amemwaga wino kuitumikia klabu ya Mbeya City fc akiungana na nyota wengine 9 waliojumishwa kikosini kwenye usajili wa dirisha dogo lililofikia tamati desemba 15.


Ngassa amesaini mkataba wa mwaka mmoja utaomuweka kwenye kikosi cha Kinnah Phiri mpaka Novemba 30, 2018,na kukabidhiwa jezi namba 10 iliyokuwa inavaliwa na Joseph Mahundi aliyetimkia Azam fc ya Dar es Salaam kufuatia kumalizika kwa mkataba wake.

Baada ya kusaini mkataba huo wa mwaka mmoja Ngassa amesema anatakakufanya kazi kwa kiwango ambacho kitaipa mafanikio timu yake mpya na kuwaziba ‘midomo’ wale wanaamini kwamba soka lake limefikia tamati.

“Najua kuna maneno na minong’ono mingi kuhusu uwezo wangu, muda si mrefu yataisha kwa sababu najua nini nataka kufanya, soka ndiyo maisha yangu, naomba watu wote walio nyuma ya timu hii waniunge mkono nina uhakika tutakuwa na majibu mazuri mwisho wa msimu” alisema Ngasa

Chapisha Maoni

0 Maoni