Kumeibuka vita ya maneno kati ya mke wa aliyekuwa mfalme wa taarab nchini Mzee Yusuph bi Leyla Rashid na dada wa msanii huyo Khadija Yusuph mara baada ya Mzee kuacha muziki wa taarab.
Khadija Yusuph aliwahi kuimba wimbo na kusema kuwa talaka inamsubiri wifi yake huyo jambo ambalo lilitafsiriwa kuwa kuwa ulikuwa ni ujumbe kwa wifi yake.
eNewz ilimtafuta Leyla Rashid ambaye ndiye mke wa mzee Yusuph na alisema kuwa hana muda wa kumtungia mtu wimbo na kwamba kwa sasa mawasiliano na mme wake ni mazuri zaidi tofauti na zamani
“Talaka inaweza kutokea kwa mwanamke yeyote aliyepo ndani ya ndoa kwa hiyo hilo siyo hata la kushangaza na mimi sina muda wa kumtafutia kiki mtu eti nimtungie nyimbo siwezi na kuhusu talaka mwenyewe Alhaji ndiye anayetakiwa kusema na siyo mtu mwingine yeyote na yaani sasa hivi mawasiliano yangu na mzee naweza sema ni mazuri zaidi kuliko hata zamani na hajawahi niambia kuhusu kumrudia Mungu na mimi naamini hayo ni maamuzi ya mtu mwenyewe na hajawahi niambia chochote” Amesema Leyla
Leyla Rashid
Baada ya Mzee Yusuph kuacha kundi la Jahazi Modern taarab ambalo lilikuwa linamilikiwa na mzee Yusuph lilivunjika na wasanii wengi kutoka na kwenda kujiunga na kundi lingine la Wakali Kwanza linalomilikiwa na Thabit Abdul na mmoja kati ya watu waliokuwa wanaunda kundi la Jahazi alikuwa ni dada wa mzee Yusuph anayeitwa Khadija Yusuph ambaye pia yeye aliondoka katika kundi la Jahazi na kwenda kujiunga katika kundi la Wakali Kwanza.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA