Tarehe halisi ya kuzaliwa kwa Yesu kristo na Chrismas halisi, kihistoria na kibiblia



Tarehe halisi ya kuzaliwa kwa Yesu kristo na Chrismas halisi, kihistoria na kibiblia

Mara nyingi na kila mtu anaamini siku ya Krismas ndiyo siku aliyozaliwa mtume wa Mungu, ama wakristo wengi wanamwita mwana wa Mungu, Yesu (kwa kiarabu nabii Issa). Swali muhimu kabisa hapa la kujiuliza ni kwamba, je ni kweli kuwa Yesu alizaliwa tarehe 25 ya mwezi Disemba? Na kama ndivyo ilivyo, je ilikuwa mwaka gani? Hapa ndipo kumekuwa na utata mkubwa kihistoria
na hata kibiblia, na mkanganyiko huu umekuwa haupati majibu halisi, maana umekuwa ukiishia kuleta mizozo tu bila suluhu.
Pamoja na mizozo hii, leo ningependa kujadili kidogo mwanga ambao unaweza angalau kujibu swali hilo, japo si kila mmoja atakubaliana na mimi.
Kibiblia, hakuna sehemu iliyotajwa kuwa siku halisi ya kuzaliwa kwa Bw. Yesu, na hata maandiko hayo ndiyo yamekuwa chanzo cha ubishani huu. Wengine pia wamekuwa wakidai kwamba, mwezi uliotajwa kwenye biblia ulikuwa katika kalenda ya kizamani ambayo kuhalisia ni sawa na mwezi Disemba kwa sasa. Pamoja na mengine mengi, makala hii pia inajaribu kulichanganua pia suala hilo la kalenda lilikuaje na ukweli wake ukoje. Lakini pia, wapo ambao wamekuwa wakidai kuwa, mara nyingi biblia haiwezi ikaeleweka kwa kuisoma vimstari vidogovidogo, sasa kwa makala hii, kwa kuwa kusudi kubwa ni kupanuana uelewa, ningependa pia mwenye ushahidi wa suala hili pengine kibiblia, basi anayo nafasi pia ku-comment kwenye blog yangu. Nimejikita zaidi kuielezea makala hii katika vitabu viwili vya injili: Mathayo na Luka, maana vitabu hivi ndivyo vimeeleza kwa undani.
Luke 1:26 & 27 “…And in the sixth month, the

cherub Gabriel was sent from the
presence of Elohim to Galilee to the
city whose name is Nazareth,
27 to a virgin who had been
betrothed to a man whose name was
Joseph, of the house of David and the
virgin's name was Mariam…

Katika mistari hii miwili ndani ya biblia, ni dhahiri kwamba, mimba ya Yesu ilitungwa mwezi Juni, mara baada ya malaika kumjia bikra Mariamu. Kwa kawaida, kutoka mwezi Juni hadi miezi tisa (kama kawaida ya ujauzito), inaangukia mwezi March, au kwa tafsiri nyingine ni kwamba, kuna uwezekano mkubwa kubwa kuwa,Yesu alizaliwa mwezi wa tatu. Kama ndivyo, je sisi tumeutoa wapi mwezi wa kumi na mbili kama mwezi aliozaliwa mtume wa Mungu Yesu? Nilipokuwa nikijaribu kuitengeneza hoja yangu kwa jamaa mbalimbali, wakaleta hoja nyingine kuwa, miezi ya zamani haikuwa sawa na sasa hivi.

Kuhusu suala la kalenda na miezi ya zamani na sasa hivi, ilikuwa hivi.

Mara nyingi kalenda iliyokuwa ikitumika ni ya kirumi na kalenda hiyo ilikuwa na miezi kumi peke yake. Miezi hiyo kumi katika kalenda ya kirumi ilikuwa inaanzia March hadi Disemba, lakini Januari na February haikuwepo. Kutokana na kipindi cha mabadiliko yaliyoukumba ulimwengu, yaliathiri hadi hiyo kalenda ya kirumi na hivyo miezi miwili mingine iliongezwa ili kukamilisha matakwa sahihi ya kinajimu (astronautic rebirth). Miezi hiyo-januari na februari iliongezwa mwishoni mwa Disemba, na hivyo kuleta mtiririko wa kuanzia march hadi februari, yaani kwa lugha nyepesi, februari ilikuwa ndiyo mwezi wa kumi na mbili kwa kalenda hiyo baada ya kufanyiwa mabadiliko. Sasa basi kama ni mwezi wa sita wa mwaka ndiyo ulikuwa mwezi wa kutungwa kwa mimba ya Yesu, na mwezi wa sita ya mwaka kwa kalenda ya kirumi na mabadiliko yake, basi ulikuwa ni mwezi August. Kutoka August hadi miezi tisa ya mimba, basi Mariamu alimzaa Yesu mwezi Juni, na hivyo krismas ilitakiwa iwe mwezi Juni. Swali ni je, tumetoa wapi Disemba kama mwezi wa kuzaliwa kwa Yesu?

Dhumuni la makala hii ni kujaribu kuelimishana masuala anuai ya baadhi ya mambo ambayo jamii inatakiwa ijifunze, siyo kuchukua kila kitu, hata kama ni cha kimungu na kukufanya kuwa cha kibinadamu, hizi ndizo dhambi tunazokutana nazo: tunasherehekea krismas kama siku ya kuzaliwa kwa Yesu, wakati kiuhalisia si siku sahihi.

Usikose kusoma Makala zangu kwenye blog hii ya husseinjuma.blogspot.com na utajifunza mengi.
Kama una maoni ama ushauri, wasiliana moja kwa moja na blogger wako kwa nambari +255759947397 kwa ujumbe ama kwa kupiga simu moja kwa moja. Makala ijayo ni kuhusu mwaka wa kuzaliwa kwa Yesu, tafadhali usikose...

Chapisha Maoni

0 Maoni