Geita. Watu sita wamefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso eneo la Kanegere, Kata ya Bukandwe, Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.
Ajali hiyo imetokea jana saa 9.30 alasiri.
Habari zilizopatikana usiku huu, zinadai kuwa miongoni mwa watu waliofariki ni Padri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Kahama ambaye aliwabeba abiria wanaosemekana ni waumini wa kanisa hilo ambao baadhi yao pia wamefariki dunia.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Salum Ndimu amekiri kupokea maiti wanne na majeruhi wanane.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA