
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akimuangalia Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji akitia ubani kama ishara ya Kuyafungua Maluid matukufu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) Sherehe zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja.

Waislamu na Wananchi waliohudhuria katika sherehe tukufu ya Maulid ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja,

Ustadh Ali Muombwa Hassan wa Chuo cha Kiislamu akitoa Tafsiri ya Qur’aan Tukufu ya Suratul Touba (Aya 128 hadi 129) iliyosomwa katika sherehe tukufu ya Maulid ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja

Wanafunzi wa Madressa Hidayatul Munineema na Nurul Islamia ya Mpendae Mjini Unguja wakisoma Qaswida YaRabii Swali katika sherehe tukufu ya Maulid ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja,

Ustadh Mohamed Khamis Rashid wa Kiweani Pemba akisoma maulid Barzanji mlango wa kwanza katika sherehe tukufu ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja, [Picha na Ikulu.] 12/12/2016

0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA