Mbunge Ridhiwani Kikwete |
MBUNGE wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na wataaluma wa Halmashauri ya Chalinze katika kuboresha mradi wa maji wa Wami kwa ajili ya wananchi wa Chalinze .
Akizungumza baada ya kutembelea mradi huo jana mbunge Kikwete alisema kuwa mradi huo ambao ulianzishwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Dkt Jakaya Kikwete ambae ni rais mstaafu wa awamu ya nne ni mmoja kati ya miradi bora iliyoleta ukombozi mkubwa wa upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa mji wa Chalinze .
Hivyo alisema kusudi la kufanya ziara katika eneo la mradi huo mto Wami ni kuona shughuli mbali mbali zinazofanywa na wataalam kwa ajili ya kuendelea kuboresha mradi huo ili kuwawezesha wananchi wake kupata huduma ya uhakika ya maji safi na salama wakati wote .
" Mradi huu uliletwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo la Chalinze mh Dkt Jakaya kikwete ni mradi ambao ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa jimbo la Chalinze na niwapongeze sana wataalam wa Halmaszhauri kwa kazi nzuri wanayoifanya ya uboreshaji wa maradi huu" alisema mbunge Kikwete
Alisema kuwa amefurahishwa na jitihada zinazoendelea kufanywa na wataalam wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wananchi wanapata maji na kazi kubwa yake mbunge akiwa ni mwakilishi wa wananchi ni kuendelea kuisimamia serikali kwa kuwawakilisha wananchi wake vema bungeni.
Huku akiwataka wananchi kuendelea kutunza miundo mbinu ya maji ili kuwezesha mradi huo kuendelea kuwa msaada kwao .
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA