Afisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema, wameamua kuupeleka mchezo mpaka Januari Mosi kwani Uwanja wa Uhuru utatumika kwa ajili ya sherehe za kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka mpya 2017.
Ameongeza kuwa mara baada ya mchezo huo ligi itasimama kwa muda wa wiki mbili kupisha Michuano ya Kombe la Mapinduzi itakayoanza kutimua vumbi Januari Mosi mwakani Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar
Mbali na mechi hiyo pamoja na mechi nyingine ambazo tayari zimekwishapanguliwa kwenye ratiba, Bodi ya Ligi italazimika kupangua ratiba ya mchezo wa Simba na Yanga uliokuwa umepangwa kuchezwa Februari 17 mwakani kutokana na wiki hiyo Yanga kupangwa katika ratiba ya mchezo wa Klabu Bingwa barani Afrika.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA