November 24 2016 Mkuu wa mkoa wa Dar es salam, Paul Makonda ameendelea
na ziara yake ya siku 10 ambayo lengo ni kukutana na wanannchi kwa ajili
ya kusikiliza kero zao. Ilikuwa ni zamu ya Ilala na hapa ulikuwa ni
mkutano wa hadhara Chanika, katika mkutano huo ulitawaliwa na kero kubwa
moja ambayo ni suala la ardhi.
Moja ya kero iliyowasilishwa ni kuhusu mwenyekiti wa mtaa wa Zavala
ambaye anatuhumiwa kuuza ardhi kinyume cha sherialikiwemo eneo
lililotengwa kwa ajili ya kuhamishia wananchi wa kata ya Kipawa ili
kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege.
RC Makonda baada ya kuwasikiliza baadhi ya wajumbe wa serikali ya mtaa
waliotoa ushuhuda kuhusu tuhuma hizo aliamuru mwenyekiti kukamamtwa
katikati ya mkutano. Unaweza kuangalia ilivyokuwa kwenye hii video hapa
chini.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA