Inaitwa Tit for Tat! Baada ya Ommy Dimpoz kueleza kwa kina kuhusiana na
sababu iliyopelekea wakakosana na Diamond, muimbaji huyo wa Salome,
amejibu kupitia Instagram.
Majibu ya Diamond ni ya mafumbo kiasi na tayari yamepokelewa kwa hisia
tofauti na mashabiki huku wengi wakichukizwa na kauli yake.
Ameandika:
Basi nlivyokuwa Mshamba Nikajua Mtu Mwenye Roho Mbaya na Mbinafsi Mungu
ndio Humuadhibu na Kumfelisha kwa Roho Mbaya lake ili asifanikiwe… halaf
Mwenye Roho nzuri Mungu Humlipa kwa Kumfanya afanikiwe zaidi na zaidi….
Asa nashangaa Mwenye Roho Mbaya eti Mungu ndio Kamfanikisha, halaf
Maskini ya Mungu Mwenye roho nzuri eti Miguu juu…..au pengine labda
Mwenyez Mungu kakosea kidogo kwenye Mahesabu yake..???[https://s] hii nayo ni #KOKORO ujue
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA