Baadhi
ya wakazi wa kijiji cha Mbirikiri kata ya Sedeko wilayani Serengeti
wakilia kwa uchungu kufuatia taarifa za watu wawili wakazi wa kijiji
hicho kudaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na askari wa hifadhi ya Taifa ya
Serengeti wakati wanawinda ,na mmoja kujeruhiwa ,hata hivyo juhudi za
kupata miili ya watu wanaodhaniwa kuuawa hazijazaa matunda baada ya
kukuta mizoga ya nyati na viatu vya mmoja wa watu hao katika eneo la
tukio,uchunguzi wa tuki unaendelea.
Mbunge
wa jimbo la Serengeti Marwa Ryoba akiwapa pole wakazi wa kijiji
Mbirikiri kuhusiana na taarifa ya maafa ya watu wawili na mmoja
kujeruhiwa ambaye pia anashikiliwa na jeshi la polisi.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA