RUVUMA: Mjamzito mbaroni kwa kujipasua tumbo kwa ajli ya kutaka kujiua.

POLISI mkoani Ruvuma linamshikiria Eva Kapinga (20), Mkazi wa Kata ya Mateka Halmashauri ya Manispaa ya Songea, kwa tuhuma za kumuua mtoto wake, Catherine Kapinga,mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu kisha kujichoma na kisu tumboni kwa lengo la kutaka kujiua na kumsababishia jeraha kubwa na kulazwa.



Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji, alisema tukio hilo lilitokea Desemba 1 mwaka huu ya saa 1:30 jioni katika Mtaa wa Mateka C Kata ya Mateka Tarafa ya Songea Magharibi.


Alisema inadaiwa Catherine aliuawa na mama yake mzazi Eva.


Alisema sababu za mauaji hayo hazijafahamika licha ya taarifa za awali kudai kuwa Eva alikuwa na malumbano kati yake na mama yake mzazi, Sofia Mayunga, ambaye alikuwa akimuuliza kwanini ameamua kushika mimba wakati anajua kuwa ana mtoto mdogo wa umri wa mwaka mmoja, jambo ambalo lilimkasirisha na kuamua kujichoma kisu tumboni kwa lengo la kujiua.


Kwa mujibu wa Mwombeji, Eva baada ya kujichoma kisu tumboni inadaiwa watu waliokuwa jirani walimkimbiza kwenye Hospitali ya Mkoa na taarifa za tukio hilo zilikuwa zimeshafikishwa Polisi na kwamba askari walipofika kwenye eneo la tukio wakiwa wameongozana na mganga walikuta Catherine ameshafariki dunia na baadaye walikwenda Hospitali ya Mkoa na kumkuta Eva amelezwa akiwa na hali mbaya akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.


Hata hivyo, Kamanda Mwombeji alisema wanaendelea na uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hilo na kwamba utakapokamilika mtuhumiwa Eva atafikishwa mahakamani.

Chapisha Maoni

0 Maoni