Sera ya Elimu Bure, shule za Msingi hali ni tete.

Ile sera ya elimu bure sasa imedhihirika kuwa ni kaa la moto ktk elimu ya Tanzania kiasi ya kwamba ni dhahiri kabisa itaathili utowaji wa elimu Tanzania.


Hayo yamethihirika wazi ktk kikao cha wazazi kilichofanyika leo ktk shule ya msingi ya Gongolamboto JICA ambapo wazazi wametoa shutuma kali dhidi ya serikali kwamba imekua ikinadi kutoa elimu bure wakati inapeleka fedha kiasi kidogo ambacho hakikidhi mahitaji kabisa.

Akiongea ktk kikao hicho mwalimu mkuu wa shule hiyo ambae hana muda mrefu shuleni hapo, ndg Job Ndugusa alisema kwamba kiasi kinachotolewa ni kidogo sana kiasi kwamba hakitoshi kabisa ktk kuiendesha shule.

Akitoa mchanganuo wa fedha wanazoletewa kila mwezi alisema kwamba,shule inawanafuzi zaidi ya 800 lkn kila mwezi wanaletewa kiasi cha tsh. 490,000 ambacho huwa kimetengewa kabisa matumizi yake. Alisema katika hizo fedha,mitihani ni asilimia 20 na uendeshaji ni asilimia 30. Hivyo ktk mitihani na majaribio ni kiasi kisichozidi 97000 ambazo hazitoshi kabisa kwa wanafunzi kufanya majariobio yao darasani, kununua karatasi, uchapishaji n.k. hali ambayo imepelekea wawe wanaandika mitihani ubaoni ambayo huwa chini ya kiwango.

Mwalimu wa taaluma wa sule hiyo akitoa majumuisho ya kitaaluma alisema kuwahali hiyo imesababisha kushuka kwa viwango vya ufaulu shuleni hapo kwani watoto hawapewi mazoezi ya kutosha. Akitolea mf, alisema mwaka huu walikua na watoto 115 wa darasala saba kati ya hao waliofeli ni 25 tu, hivyo wameshinda kwa kiasi cha asilimia 85. Lkn akasema ushindi huo umekua wa chini sana kwani watoto wameshinda kwa viwango vya chini vya D,C,B na kiasi kidogo sana cha A hali itakayopelekea watoto wengi kukosa kwenda sekondari tofauti na miaka na nyuma
Kutokana na hali hiyo wazazi kwa kauri moja walimuomba mwenyekiti wa bodi ndg Mkama na msaidizi wake ndg Keneth Mfinyu kuwaondoa walimu wote ili wao walijadili swala hilo kama wazazi bila kuwashilikisha walimu.

Katika maamuzi yao wameamua kwa pamoja kuchangia elimu hasa masomo ya ziada pamoja na tuisheni. Mzazi mmoja Juliasi isaya alitoa angalizo kwa wazazi wenzake kuwa wasiwasikilize wana siasa wanaosema elimu bure wakati watoto wao hawasomi shule hizo,wanawapeleka watoto wao kwenye shule za kimataifa

Wameitaka serikali isiwaingilie ktk maamuzi yao kwani wanao halibikiwa ni watoto wao wala si watoto wa Raisi, waziri,RC au DC,. Mzazi mmoja Faraja Mwitaa lisema inaonekana wazi kuwa sera hii ya elimu bure imeisha washinda serikali hivyo ni jukumu la wazazi kuingilia kati la watajikuta wamechelewa.

Tangu aingie madarakani raisi John Pombe Magufuri amekuwa anapambana kuitekeleza sera hii ambayo haikuwa sera ya chama,jambo ambalo linampa shida kubwa kuilikamilisha kwani halikua na maandalizi yoyote wala mfumo maalumu wajinsi ya kulitekeleza kiasi ambacho huumfanya wakati mwingine alalamike kuwa amepewa mzigo mzito unaomuelemea.

Chapisha Maoni

0 Maoni