Tafakuri: Huku ndiko Lwandamina anakoelekea

Kama umepata bahati ya kucheki game ya leo dhidi ya JKT ruvu na pengine game ile ya kirafiki dhidi ya JKU utakuwa kwenye nafasi ya kumuelewa mwl Lwandamina. 


Nawashauri mkiwa mnatazama game yeyote ya Dar es Salaam Young Africans SC kuweni sana na aina ya uchezaji. Mtagundua kuwa wachezaji wanapata wakati mgumu sana kutekeleza mfumo wa Lwandamina wawapo uwanjani katika dakika za awali. 

Falsafa na Mfumo wa Lwandamina kulazimisha sana viungo kuwa nguzo kuu ya upatikanaji wa Mabao. Style/Mfumo ambao umekuwa ukitumika sana Simba sports club.... na ambao pia umekuwa kinyume na style ya uchezaji wa Klabu ya Dar es Salaam Young Africans SC. 

Kama ulitazama vyema game ya Yanga dhidi ya JKT ruvu utagundua muda mwingi viungo walikuwa wakilazimika kupenyeza mipira katikati ya mabeki wa timu pinzani... 
Pia viungo ndio walikuwa responaible kusambaza mipira kwa washambukiaji wa pembeni. 

Ni tofauti sana na jinsi tulivyokuwa tukicheza tangu hapo awali. 
Ambapo mara nyingi tumekuwa tukiona mipira ikitoka kwa Golikipa - Juma Abdul - Msuva then ndio unapigwa kati kutafuta bao. Inaonekana wachezaji wamepigwa marufuku kabisa kufikisha mpira mbele bila Kiungo kuugusa/kuhusika katika mpira huo. 

Sasa unaweza ukawa umepata picha kwanini Zulu hakuwa kabisa kwenye kikosi cha leo. 

Sasa unatambua kwanini Makapu alilazimika kuingia dakika za mwisho kabisa. 

Lengo kuu ilikuwa kuangalia kama viungo wachezeshaji wanaweza kutekeleza. 

HITIMISHO:

YANGA hii itakuwa na silaha mbili za Ushambulizi. 

1. Wing Attack (Natural) 
2. Penetrative pass Attack (Lwandamina's philosophy) 

Naiona YANGA hii ikiwa bingwa wa VPL mfululizo kwa zaidi ya mara 6 mpaka 8. Kwa sababu hakuna klabu Bongo yenye silaha hizi mbili za mauaji. 

Napata shida kuifahamu klabu yeyote ambayo inaweza kuzuia hizi philosophies mbili kwa wakati mmoja....! 

Napata shida pia kujua Klabu gani hapa Afrika Mashariki ina uwezo huu. 

Napata shida kujua kama wale ambao wamecheza na Yanga(iliyokuwa na philosophy ya aina moja) kwa zaidi ya mara 5 (na kushindwa kupata uahindi) wanawezaje kuifunga hii ya sasa. 

Chapisha Maoni

0 Maoni