Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Mbao FC, Khalfan Ismail amefariki baada ya kugongana na kuanguka uwanjani.
Mechi hiyo ilikuwa inachezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ambako michuano ya vijana chini ya miaka 20 inaendelea.
Ismail aligongana na beki wa Mwadui FC wakati wakiwania mpira na kuanguka na juhudi za kuokoa maisha yake zilionekana kukakwama.
Wakati mauti yanamkuta Ismail, dakika chache kabla alikuwa amefunga bao dhidi ya Mwadui.
Pamoja na kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Kagera, taarifa baadaye zilizopatikana zilieleza, Ismail alifariki palepale uwanjani.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA