Oktoba 16, mwaka 2010, Yanga ilipambana na Simba kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Shujaa wa Yanga katika pambano hilo alikuwa ni mshambuliaji Jerson Tegete aliyefunga bao pekee na Yanga dakika ya 70.
Tukio la bao lilianzia kwa Isaac Boakye, raia wa Ghana aliyeanza mpira wa adhabu kwa haraka na kumpasia Nsa Job.
Nsa alimpa pasi ya haraka haraka Tegete ambaye aliambaa na mpira na kumtoka mlinzi wa Simba, Joseph Owino kisha akamchambua mlinda mlango, Juma Kaseja.
VIDEO YA BAO HILO
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA