Baada ya ushindi wa Simba 2-0 Ndanda, kuwa na taarifa zinazoenea kwenye mitandao ya kijamii kwamba huenda Simba ikapokwa pointi kwa kosa la kuwachezesha wachezaji wawili wa kigeni (Daniel Agyei na James Kotei wote kutoka Ghana) ambao bado hawajakamilisha vibali vya kufanyia kazi nchini.
“Niseme hizo taarifa ni za uzushi ambazo zimeletwa na wapinzani wetu ambao waliamini kwamba tutapoteza mchezo wetu dhidi ya Ndanda na wao wataendelea kuwa juu ya msimamo wa ligi kwa hiyo ushindi wetu haujawapendaza ndio maana wameamua kuendesha vita ya maneno ya uongo na uchochezi,” amenukuliwa makamu wa rais wa Simba SC Geoffrey Nyange Kaburu wakati akizungumza kwenye kipindi cha Sports Extra cha Clouds FM.
“Simba imekamilisha taratibu zote za usajili ambazo zipo ndani ya kanuni zetu za VPL, baada ya kukidhi mahitaji yote wachezaji husika walipewa leseni na TFF na ndio ambazo zilitumiwa siku ya mchezo kwa hiyo vijana wetu walikuwa na vigezo vyote vya kucheza dhidi ya Ndanda kulingana na kanuni zetu.”
“Wanachama na wapenzi wa Simba wapuuzie haya maneno, kwa sasa lengo letu ni kwenye mchezo wetu unaofata dhidi ya JKT Ruvu siku ya Jumamosi na kubwa ni kuendelea kuvuna pointi na hilo ndio kiu ya wengi kuona timu inashinda kila mechi na hatimaye kutwaa ubingwa.”
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA