Ukweli kuhusu Waraka wa Kanisa Katoliki na tarehe 09-Desemba siku ya Uhuru wa Tanganyika


image.jpeg
image.jpeg

Nilichojifunza ni kuwa wengi wamepotosha waraka huo wa Maaskofu,na pengine kwa aina ya #Pseudophilosopher kama Yericko,watu wanaweza kubeba "bandiko" lile na kuamini kuwa ni "tangazo la Kanisa" kwa "Watanzania wote".

Niliamua kuingia "maktaba" na kuangalia barua ile ya Papa ya mwaka 1984 iliyofahamika kama "Tot Tantaeque",iliyoandikwa kwa Kilatini.Barua ile iliandikwa kwa Rais wa TEC wakati huo akiwa Muhashamu Antony Mayala(Askofu wa Jimbo la Musoma).Nimeimbatanisha hapa barua hiyo ya Papa ya mwaka 1984.

Papa anamuandikia Askofu Mayala,na kumuomba ahakikishe Kanisa linadumisha amani ya nchi,anasisitiza upendo na mshikamano ndani ya Taifa changa la Tanzania;na kwa imani ya kanisa,Papa analiweka Kanisa la Tanzania na Wananchi wake ambao wanaamini katika imani ya Kanisa Katoliki chini ya Usimamizi wa Bikiara Maria Imakulata(Mkingiwa dhambi ya asili).

Hili jambo si la "Taifa",hili jambo ni la Kanisa,tena Kanisa Katoliki,wala halihusiani na "siasa" za vyama wala mambo ya kidunia,bali mpango na imani ndani ya utaratibu wa kanisa,kuwa kila nchi huwa na msimamizi wanayemfuata kama Patron.

Tukichukua mfano wa "kidunia" hii ni kama mlezi;Yaani kule CCM unamkuta Asas na uzee wake ni "mlezi" wa UVCCM mkoa wa Iringa,Marehemu Samuel Sitta alikuwa mlezi wa chama Mkoa wa Njombe(?).Wakati Kingunge alikuwa "mlezi" wa UVCCM na kamanda wao Kitaifa.

Katika kanisa utaratibu huo upo;ndio maana watu kama Mtakatifu Fransisko wa Asisi huyu ni mlezi wa Watunza wanyama pori na wanaikolojia,sababu maisha yake yalikuwa ni kutunza wanyama.Mtakatifu Kizito sbb ya utoto wake wakati akiteswa na Kabaka,basi huyu ni msimamizi wa watoto wa shule nk.

Kwa kawaida kwa utaratibu wa kanisa katoliki kila nchi huwa na msimamizi wake(Patron/Matron).Usimamizi huu hautahiri imani za watu wengine na wala hazilazimishi wewe usiyekuwa mkatoliki kuamini hivyo.Hii ni kwa wakatoliki na utaratibu wao.Ukienda Uturuki wana msimamizi wao,India,Pakistani,China na hata Japan.Hivyo Tz sio ya kwanza na wala haitakuwa peke yake


Kuna upotoshaji kuwa barua ile imeelekezwa kwa Rais wa JMT kisa pale juu pameandikwa "President".Huu ni upotoshaji.Muundo wa Baraza la Maaskofu Tz upo kama hivi:Rais wa TEC,Makamu wa Rais wa TEC,Katibu wa TEC(Ambaye ndio mtendaji wa kila siku;cheo kilichowahi shikwa na Dr Slaa),na ndani ya TEC kuna idara mbalimbali kama Idara ya Uinjilishaji,Idara ya Mawasiliano,Idara ya Sheria na Haki nk.

Sasa barua ile ilitoka kwa Rais TEC(Department -President) kwenda kwa maaskofu wakuu na Maaskofu ili iweze kuwafikia waumini wote wakatoliki Tanzania.na si kwamba ilikuwa inapelekwa kwa Rais wa JMT.Haya mambo ya "imakulata" ni mambo ya "dogma".Hulazimishwi kuamini sababu ni mambo yanayohusu imani ya watu na watu.Its a dogmatic point of reference...Just handle it or hold it..

Hapo Rwanda,msimamizi wa Taifa lao ni "Kristo Mfalme",Italia wao ni Fransisko wa Asisi,Ufaransa ni Mt.Dionis(Denis) na ndio maana uwanja mkubwa wa mpira pale Paris uliochezwa fainali mbili za kombe la dunia unaitwa St.Dionis Stadium.Huyu ndio msimamizi wao na sisi Tanzania ni BM wa Imakulata.

Sasa ukipata #pseudophilosopher kama Yericko Nyerere,basi anaweza kutumia hoja hiyo kupemyeza "mambo" yake bila kutoa nafasi kubwa ya kufafanua,hivyo kuzusha yale yale ambayo wengi huamini kwa sababu hawana taarifa kamili.

Sikukuu ya BM Imakulata haijaanza mwaka 1984 pale Papa alipoandikia barua kwa TEC,Sikukuu hii ilianza toka mwaka 1570's,na ni sikukuu ya Kanisa Katoliki Ulimwenguni,na huandimishwa 08/Dec.

Sasa kwa vile Waumini Wakatoliki wa Tanzania ambao pia ni Watanzania huwa wanaungana na Watanzania wa madhehebu tofauti kusherekea kumbukumbu ya Uhuru 09/Dec ya kila mwaka.Kanisa Katoliki la Tz limeamua rasmi,badala ya kusherekea sikukuu hiyo ktk kalenda ya Kanisa ya 08/Dec wao wameamua kuipeleka 09/Dec ili kupata fursa ya kuiombea na nchi ktk siku taifa lilipopata uhuru.

Hii si lazima kwa wewe mpagani,bohora,Muislamu,Msabato,Mlutheri na yule muanglikana.Hii ni kwa kalenda ya Kanisa Katoliki Tz,ambalo kama ilivyo kwa nchi nyingine duniani wao pia huwa na siku ya kumbukumbu wa "msimamizi wao kikanisa" ndani ya nchi yao.Hawa ma #pseudophilosopher wasituingize ktk malumbano ambayo ufafanuzi wake unahitaji uelewa wa kawaida tu wa mambo ya kanisa.

Chapisha Maoni

0 Maoni