Rais wa Marekani Donald Trump anajiandaa kuwahutubia viongozi kutoka Mataifa 40 ya kiislamu, kama sehemu ya ziara yake nchini Saudi Arabia.
Akihutubia kongamano la mataifa hayo ya kiislamu katika mji mkuu Riyadh, anatarajiwa kutoa wito wa pamoja wa kukabiliana na imani ya itikadi kali.
Bwana Trump alianza siku ya leo kwa kufanya mikutano na viongozi wakiwemo marais Abdul Fatah el Sisi wa Misri na Mfalme wa Bahrain.
Mwaandishi wa habari wa BBC wa maswala ya usalama amesema kuwa Bwana Trump, yumo katika eneo hatari, na faida ya mkutano huo itategemea na namna atakavyozungumza na kilichomo kwenye hotuba yake.
Hatua yake ya hivi majuzi ya kupiga marufuku safari ya kwenda Marekani kwa raia wa mataifa 7 yenye waislamu wengi duniani, ilisababisha hasira kote katika mataifa ya kiislamu.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA