Ni Mdee tena: Awakalia kooni wabunge wa CCM, awataka wasome ilani yao vizuri

Mbunge Halima Mdee leo akiwa bungeni amewataka wabunge wa Chama Cha Mapinduzi vijana hata wale watu wazima lakini hawana muda mrefu bungeni wasome vizuri Ilani ya Uchaguzi ya CCM na mpango wa maendeleo kabla ya kusimama bungeni na kuanza kutoa sifa.

Halima Mdee amesema hayo bungeni leo wakati akichangia katika bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi baada ya wabunge wengi wa Chama Cha Mapinduzi kusimama na kuanza kusifia Wizara hiyo kuwa imepiga hatua baada ya kufuta tozo nyingi jambo ambalo Halima Mdee anasema ni jambo dogo sana ukilinganisha na changamoto ilizonazo Wizara hiyo ambayo kila mwaka imeonekana kushuka katika sekta ya kilimo ambacho ndiyo uti wa mgongo wa taifa.

Kufuatia jambo hilo Halima Mdee amewataka wabunge wa CCM kusoma vizuri Ilani ya Uchaguzi waone inasema nini na inataka nini lakini pia wasome na mpango wa maendeleo ili kuona changamoto ambayo Wizara hiyo inayo.

"Nimeona wabunge wengi vijana hata wale watu wazima wakisimama na kutoa pongezi kwa Waziri kisa tu amepunguza tozo, lakini ndugu zangu tozo pekee ni kitu kidogo sana lakini hata Waziri alitumia muda wake mwingi jana kuhusiana na tozo tu, ndugu zangu Wabunge wa CCM mkasome vizuri Ilani ya Uchaguzi ya CCM, mkasome na mpango wa maendeleo, hapa hatutafutiani ubaya kwani mafanikio yenu nyinyi ndiyo mafanikio yetu sisi pia, kwa hiyo tusichukiane tunasema haya kwa dhamira njema, ukichukua kitabu cha Wizara ya Kilimo na kile cha Wizara ya Viwanda haviendani yaani ni kama mbigu na dunia" alisema Halima Mdee

Chapisha Maoni

0 Maoni