Kwa mujibu wa tovuti ya Tanzania Today na Dewjiblog
Usiku wa Alhamisi ya Novemba, 17 kumefanyika halfa ya utoaji wa tuzo ya
Forbes Person Of the Year kwa mwaka 2016 ambazo zilikuwa
zikiwashirikisha watu watano kutoka mataifa mbalimbali Afrika.
Mmoja wa washirki wa tuzo hizo alikuwa ni Rais wa Tanzania, Dkt. John
Magufuli ambaye alikuwa akishindana na Michiel Le Roux – mwanzilishi wa
benki ya Capitec ya Afrika Kusini, Thuli Madonsela – mwanasheria na
mtetezi wa haki za binadamu wa Afrika Kusini, Rais wa Mauritian, Ameenah
Gurib na watu wa Rwanda.
Katika halfa ya utoaji wa tuzo hizo, Mwanasheria na mtetezi wa jamii wa
Afrika Kusini, Thuli Madonsela ametajwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Forbes
Person of the Year 2016 kutokana na juhudi zake anazozifanya za kusaidia
jamii ya watu wa Afrika Kusini katika mambo mbalimbali yakiwepo ya
kisheria.
Thuli Madonsela anakuwa mshindi wa sita wa tuzo hizo tangu zianzishwe
mwaka 2011, washindi waliopita walikuwa ni Sanusi Lamido Sanusi – 2011,
James Mwangi – 2012, Akinwumi Adesina – 2013, Aliko Dangote – 2014 na
Mohammed Dewji – 2015.
Kwa kushindwa huko kwa Rais Magufuli, Mohammed Dewji ambaye ni
Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa Makampuni ya Mohammed Enterprises
Tanzania Limited (MeTL Group) anasalia kuwa Mtanzania pekee ambaye
amewahi kushinda tuzo hiyo
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA