.
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ameitaka Uganda kubadili jina la Ziwa Victoria ili liendane na jina linalowakilisha uhalisia wa wananchi wa eneo hilo.
Kiongozi huyo anayekosolewa vikali nchini mwake amesema tayari amemfahamisha Rais Yoweri Museveni juu ya haja ya kubadilishwa jina hilo.
Jina la Ziwa Victoria lilitolewa na mtafiti mmoja wa Uingereza kama zawadi kwa Malkia wa Taifa hilo aliyetambulika kwa jina la Victoria.
Akizungumza katika ufunguzi wa maonyesho ya utalii mjini Kampala, Rais Zuma amesema Ziwa hilo kuendelea kuitwa Victoria kunawanyima fursa wananchi wa eneo hilo kujivunia uasili wao.
“Mnaweza kuweka bango kubwa linaloonyesha jina la jipya na kisha mkaweka bango dogo litakalosomeka kama “ zamani eneo hili liliitwa Ziwa Victoria”. Lazima mbadilishe jina hili na kuweka jina litakaloelezea uzuri wa Taifa hili,” amesema Rais Zuma.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA