Baada ya kusemekana amepigwa chini Azam Fc, Saad Kawemba afunguka haya

Baada kuenea kwa taarifa za Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawemba kupigwa chini, mwenyewe ameibuka na kueleza kinachoendelea ndani ya klabu hiyo.


Kawemba ameeleza kuwa bado anaendelea na majukumu yake ndani ya klabu hiyo, lakini mkataba wake unaelekea ukingoni huku akiwashangaa wanaoeneza taarifa hizo.

“Unajua watu wanasema mengi, lakini kiukweli hakuna mtu aliyenifukuza Azam, kwa sababu hivi sasa natoka zangu ofisini naelekea Chamazi, sasa inawezekanaje nifukuzwe halafu bado niendelee kuwepo katika ofisi zao? Nasikia mengi maana hata nilivyokuwa TFF mengi yaliongelewa, hivyo hakuna kipya.

“Lakini pia wanatakiwa kujua kwamba nafanya kazi kwa mkataba ambao unaelekea ukingoni na utamalizika mwezi huu na hiyo ni kawaida kwa mtu yeyote mkataba unapoisha lazima aondoke au abaki, siyo kwangu tu, na tupo katika mazungumzo, kama yakienda vizuri nitaongeza mkataba,” alisema Kawemba, jana.

Chapisha Maoni

0 Maoni