Bungeni: Joseph Msukuma Asema Ana Majina ya Wabunge wa Upinzani Waliohongwa Kuitetea ACACIA


Kwa kipindi kifupi kilichopita bunge letu lilianza kurudi kwenye misingi ya kizalendo, ila tokea hii budget ya madini ianzwe kusomwa vijembe,majigambo,maneno ya kuudhi,kejeli zimerejea mahali pake.

Leo kwa mara nyingine mbunge wa Geita, mh Msukuma aliomba dakika za nyongeza kutoka kwa Hawa Ghasia na kuwashambulia wabunge wa upinzani badala ya kuzungumza hoja. 

Mh. Msukuma alisema wapinzani wamehongwa na anawajua ingawa hakuwataja, pia akasema Msigwa anamiliki nyanya,kuku na mbwa hawezi jua mambo ya madini kama vile haitoshi akamrudia Mnyika kwamba anamiliki mchanga wa matofali.

Chapisha Maoni

0 Maoni