Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Felix Ngamlagosi kuanzia leo tarehe 11 Juni, 2017.
Maamuzi haya yamekuja siku mbili baada ya habari za kampuni ya IPTL kutaka kuongezewa mkataba wa uzalishaji umeme ambapo pia Kituo cha sheria na haki za Binadamu kilijitokeza na kusema hakikubaliani na mkataba huo kuongezwa kwani kampuni hiyo inahusishwa na kashfa ya uchotwaji wa Mabilioni kupitia account ya ESCROW.
Hata hivyo baada ya kituo hicho cha LHRC kujitokeza kuongea, EWURA walijitokeza na kusema "Kuna vitu viwili vya kuzingatia hapa, EWURA tunachodili nacho sasa hivi ni leseni ya IPTL ambayo aliipata 1996 ikiwa ni ya miaka 21 na inaisha July 2017"
“Sheria iliyoanzisha EWURA na sheria ya UMEME zinataka mtu yeyote anavyoomba leseni EWURA itoe taarifa kwa umma ili watu watoe maoni au pingamizi, hicho ndicho tulichokifanya na hatuendi kwa siri…. tumetoa siku 21 za kupokea maoni, kinachotendeka hapa ni IPTL kutaka kuomba kuongeza leseni"
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA