Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa ameagiza maafisa mifugo kote nchini kuhakikisha wanafanya sensa ya mifugo na kuwataka wafugaji kuhakikisha wanafuga kulingana na eneo la kulisha ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima kwakuwa serikali imedhamiria kuwasaidia wafugaji.
Waziri Mkuu ameyasema hayo katika ziara wilayani Gairo ambapo amewataka viongozi kuhakikisha wanatoa elimu kwa wafugaji kufuga kwa uwezo wa ardhi uliopo ili kuepuka wafugaji kulisha katika mashamba ya wakulima.
Aidha Waziri Mkuu katika ziara hiyo ametembelea miradi ya maji ya Chakwale, Magoeko ambayo imejengwa muda mrefu bila ya kuwa na mafanikio kwa wananchi huku akiwataka wataalamu wa maji mkoani morogoro na wilayani Gairo kuhakikisha wanafanya kazi kwa ufanisi ili kutatua kero hiyo.
Naye Waziri wa maji Gerson Lwenge amesema kuwa wameshatenga bajeti
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA