Jeshi la Polisi Manyara linamshikilia Mbunge Mary Nagu kwa amri ya Mkuu wa Wilaya

Mbunge wa Jimbo la Hanang, mkoani Manyara Dkt Mary Nagu (CCM) na mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo jana walikamatwa  na Jeshi la Polisi wilayani humo kwa amri ya Mkuu wa wilaya hiyo kutokana na sababu ya  kushindwa kuelewana kiutendaji.

Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya Sarah Msafiri ameeleza kuwa aliagiza kukamatwa kwa Mbunge huyo baada ya kuchoka kumvumilia kutokana na kauli anazozitoa kwenye mikutano yake na wananchi akihamasisha wasishiriki shughuli za maendeleo.

Pia amemtuhumu Mbunge huyo kuwataka wananchi wasishirikiane naye jambo ambalo alidai ni sawa na kuwataka wananchi wasishirikiane na serikali kwa sababu yeye anasimama kama serikali

“Ni kweli tumemkamata na sababu kubwa ni kuhamasisha wananchi wasishiriki shughuli za maendeleo na pia anawataka wananchi wasishirikiane na Mimi wakati anajua Mimi nasimama kama serikali” -DC Msafiri

Chapisha Maoni

1 Maoni

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA