Naibu Wazri Ikupa atekeleza ahadi yake

Naibu Waziri wa sera, Bunge, Kazi, vijana, ajira na walemavu Mh Stella Ikupa leo amefanya ziara ya ya kutembelea shule ya Sekondari Jangwani, Uhuru Mchanganyiko na Pugu jiji Dar es salaam na kukabidhi  vifaa mbalimbali kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu  .


Katika ziara hiyo Mh, Ikupa ametoa Magongo ya kutembelea, viti mwendo, fimbo nyeupe kwa wasiona, miwani ya jua, kofia, lenzi za kusomea kwa watu wenye uono hafifu, na ualubino ili kutatua changamoto kwa kundi hilo maalumu.


"Sisi kama serikali tunatambua changamoto hizi hivyo tunajitahidi kukabiliana nazo na kidogo kinachopatikana tunakigawa kwa kila mmoja ili kupunguza matatizo haya kidogokidogo na mwisho wa siku yataisha" amesema Naibu Wazoiri  Ikupa

Pia serikali hii inayoongozwa na Rais Magufuli itaendelea kutennga fedha kwa ajili ya kuendeleza kuwahudumia watoto wenye ulemavu hivyo kikubwa tuendelee kushirikiana ili kwa pamoja tutatue changamoto hizi kwa kundi lenye lenye mahitaji maalumu kwa kadri iwezekanavyo


Hata hivyo ametoa wito kwa wanafunzi hao wenye mahitaji maalumu kujikita kwenye elimu ndio mkombozi wa maisha yao kwani pasipo na  elimu au ujuzi wowote wanaweza kurudi mtaani na kuwa ombaomba, pia kutokana na serikali hii kuwa sikivu tunaendelea kuboresha miundombinu kwa kukarabati kadri siku zinavyoenda na isiwe tena kuwa kikwazo cha kukosa elimu.

Aidha Makamu mkuu wa shule ya Jangwani Eunsta Siara akisoma taarifa mbele ya  Mh, Ikupa amesema kuwa kundi hilo lina changamoto mbalimbali ikiwa pamoja sehemu ya maabara sehemu za kulala walemavu, majengo hivyo kama serikali isaidia kukamilisha vitu hivyo ili pasiwe na kikwazo cha kukwamisha elimu kwa kundi hilo maalum.

Cosmas Antony ambae ni mwanafunzi wa Kidato cha tatu  Pugu sekondari amefurahi na kumpongeza Mh, Ikupa kwa kutekleza ahadi yake kwani aliahidi kwani mwaka jana aliahidi kuleta vitu ambavyo vitasaidia kurahisishia mazingira ya kupata elimu bora na amefanya hivyo.

Chapisha Maoni

0 Maoni