RAIS MAGUFULI ASIKITISHWA SANA NA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU

Hii  ni kutokana na baadhi ya vyombo vya kutetea haki za binadamu kudai kuwa hatua ya Mheshimiwa JPM maarufu kama kutumbua majipu kwa kuwatangaza hadharani kunakiuka haki za binadamu.

"...nimesikitika sana kwa baadhi ya vyombo vya kutetea haki za binadamu kwa kile wanachodai kukiukwa kwa haki za binadamu kwa kuwatangaza hadharani wanaowaibia watanzania, sasa najiuliza, au na wenyewe [vyombo vya kutetea haki za bindamu] ni majipu..." anasema DKT JPM,

Katika hatua nyingine, rais ameendelea kuonesha msimamo wake wa kurejesha maadili ya uongozi na kuendelea kutumbua majipu kwa manufaa ya watanzania wa hali ya chini.

Makamu wa rais, Bi Suluhu pia amesema ataunga mkono hatua ya rais JPM ya kutumbua majipu ili kurudisha hadhi ya chama na kulinda maslahi ya wananchi wa hali ya chini.

Chapisha Maoni

0 Maoni