'FROG' MWINGINE WA SNURA DODOMA AUTAKA UBUNGE SOCTE

Mwalimu-mwanafunzi chuo kikuu cha Dodoma na aliyewahi pia kunengua na kuonesha mauno jukwaani mbele ya halaiki kwenye Tamasha la KICHUO ZAIDI CONCERT lililotumbuizwa na mwanamziki Diamond na Mafikizolo tarehe 12 May kwenye viwanja vya COED, chuo kikuu cha Dodoma SARAH TABARO sasa yupo kwenye kampeni za kukata na shoka kuutaka uwakilishi(ubunge) wa SCHOOL OF CURRICULUM AND TEACHER EDUCATION (SOCTE). Angalia hapa mwalimu huyo akikata mauno na Diamond


Leo pia mgombea CHURA amefanya kampeni zake 'theatres' huku mavazi yake yakiendelea kuonesha mmomonyoko mkubwa wa maadili na kwa taarifa za kuaminika toka katika chanzo chetu zinataarifu kuwa, walimu walio na maadili walimtaka kwenda kubadili kwanza nguo ili arudi aombe kura; ni aibu nyingine kwa CHURA
.

Jana pia alifanya kampeni zake huku umati wa watu ukisikika kumuomba awape kidgo, '...tupe kidogo...', yaani anengue kidogo kama alivyonengua jukwaani, na bila kujali mgombea huyo aliwapa kidogo kwa kutikisa, huku umma mkubwa ukimshangilia.

Hadi sasa, bado wagombea wanaendelea kuchuana vikali kwa uchaguzi utakaofanyika hapo kesho jumamosi ya tarehe 21 May ili wanachuo kuamua hatima ya uongozi wao kwa njia ya kura.

Chapisha Maoni

0 Maoni