Mbowe ajumuika na wakaguzi wa shule kukagua shule ya sekondari Harambee.

Mbunge wa jimbo la Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe, ameongozana na Wakaguzi wa shule wa Kanda Mkoani Kilimanjaro na Afisa Elimu Wilaya ya Hai na Diwani wa Machame Mashariki kukagua bweni la shule ya Sekondari ya Harambee iliyopo Machame wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.


Bweni hilo la kisasa lilojengwa kwa jitihada za Mbunge wa Hai kwa kushirikiana na Diwani na wadau mbalimbali wa Elimu kutoka Mkoa wa Kilimanjaro, lina ghorofa mbili huku likiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 181 kwa wakati mmoja.

Wanafunzi wenye sifa za kuendelea na kidato cha V na VI lakini walikosa nafasi wataandikishwa na kuendelea na masomo katika shule ya Harambee, sera ya Serikali inataka ili shule iwe na sifa ya kuwa na kidato cha V na VI lazima iwe na bweni.

Elimu ni kitu muhimu, wakati wa sasa bila kuwapatia watoto elimu bora, na kuandaa mazingira bora ya kuwapatia elimu, ni wazi tunawaandalia wakati mgumu katika maisha yao siku za mbele, jamii haina budi kuhakikisha watoto wanapata elimu, kila mmoja ashiriki kuhakikisha elimu inapatikana, kila Mwenye nafasi fulani ajitahidi kuhakikisha watoto wanapata elimu.

Tukiwa na Taifa lenye wasomi wa kutosha uzalishaji wa bidhaa zilizo bora utakuwepo, uchumi utakuwa kwa wastani unayostahili, kila mmoja akipata kipato kichafanya ajiletee maendeleo yake na jamii kwa ujumla.

Kila mtu atoe kipaumbele katika elimu, 1. Iwe elimu, 2. Iwe elimu na 3. Iwe elimu, elimu kwanza kwa Taifa lenye ustawi thabiti na Imara.
 

Chapisha Maoni

0 Maoni