VODACOM KICHUO ZAIDI CONCERT NA BALOZI WA VODA "PLATINUMS" PAMOJA NA MKALI WA MASAUTI TOKA AFRIKA KUSINI MAFIKI ZOLLO NDANI YA UDOM.

Hili ni tamasha la kipekee lililoandaliwa na kampuni ya maawasiliano ya vodacom ambalo limewaleta wakali wawili wa muziki wa kisasa: mkali wa bongo flavour nchini na balozi wa Vodacom Abdul Nasseeb (Diamond) na mkali wa masauti mtoto wa kizulu toka Afrika ya kusini Mafiki Zollo, limefanyika chuo kikuu cha Dodoma katika viwanja vya COED leo alhamisi tareheh 12 May.

Sambamba na wakali hao wawili, waziri Nnauye na January Makamba pia alikuwa katika viwanja hivyo kushudia tamasha hilo bab kubwa.

Mafuriko ya watu yalionekana kuanza kutia nanga katika viwanja hivyo tangu ilipotimu saa kumi jioni katika viwanja hivyo vilivyoonekana kupambwa toka jana kama sehemu ya maandalizi.

Chapisha Maoni

0 Maoni