LISU: ALICHOKIKATAA BABA WA TAIFA, SERKALI YA TANZANIA IMEKIFANYA KWA MUDA WA MIAKA 20.

Akichangia hotuba yake Bungeni kama msemaji mkuu wa kambi rasmi ya upinzani, kamanda Lisu amemnukuu baba wa taifa juu ya kile alichojibu akiwa uingereza mwaka 1981 juu ya adha ya muungano na kusema kwamba, endapo umma wa wazanzibar utaona hakuna haja ya kundelea na muungano, asingewalazimisha kwa kuwapiga mabomu.

Sikiliza dk 20 za kamanda lisu hapa.

Vilevile kamanda Lisu amesema, Zanzibar imekuwa koloni kwa miaka kadhaa kwa koti la muungano ambapo imetawaliwa kijeshi, kisiasa na kiuchumi huku serikali ya Tanganyika imekuwa ikiamua ni
nani awe rais na nani hastahili kuwa rais wa Zanzibar.

Katika hatua nyingine, Lisu amewavaa mawaziri wa serikali ya awamu ya tano ambao wanafanya kazi na kutumbua majipu bila hata ya JOB DESCRIPTION, ambapo ni kinyume kabisa cha sheria na hivyo ametoa ushauri kwa waliotumbuliwa majipu wana haki ya kwenda mahakamani na kudai kusitishwa kutumbuliwa kwao majipu kwani waliowatumbua hawakufanya kazi kisheria.

Chapisha Maoni

0 Maoni