SANAA YETU YA KITANZANIA: KWA NINI WASANII WA KIKE WASIWE KAMA LADY JAY DEE?

Linganisha hizi nyimbo mbilil kisha ujue kwa nini namkubali Lady Jay Dee...!

Nimefikiria sana kuhusu sanaa zetu na maadili halisi ya wasanii, na kwa muda mrefu nimekuwa nikimfuatilia kwa ukaribu sana msanii Judith Wambura al maarufu
kama Anakonda. Binafsi namchukulia Jide kama ROLL MODEL kwa wasanii wa kike nchini, na kwa maadili yake, nafurahi kujifunza sanaa yake.

Wito wangu kwa wasanii wa kike nchini, kwa nini wasiige maadili na mienendo ya msanii huyu na si kutoa nyimbo ambazo kwa uhalisia zinaporomosha maadili ya kizazi cha kesho? Kuna umuhimu gani ya kutoa wimbo nje ya maadili kama wimbo alioutoa Snura ule wa chura, hivi jamii yetu inajifunza nini kutoka kwa wasanii kama hawa? BASATA, kazi yenu hasa ni nini?

Chapisha Maoni

0 Maoni