SHINYANGA, UNAMKUMBUKA SHELEMBI? PIATA HAPA

Miaka kadhaa sasa tangu atutoke kamanda wetu kipenzi, hayati Philip Magadula Shelembi ambaye kifo chake cha utata kilitokea mnamo tarehe 26 Aprili 2011 katika hospitali ya mkoa Shinyanga. Vyanzo mbali mbali vilieleza kwa hisia tofauti tofauti juu ya kifo cha kamanda huyu aliyeiinua CHADEMA kwa Shinyanga hasa katika uchaguzi wa mwaka 2010 ambapo kamanda huyu kiukweli alipigania sawasawa na matakwa ya walala hoi maana naye pia alikuwa ni mlala hoi halisi.

Buriani Shelembi!
Leo nimekaa na kumkumbuka kamanda huyu katika harakati zake wakati pia alikuwa ni mgombea nafasi ya ubunge jimbo la Shinyanga mjini ambapo kwa kweli binafsi huwa nafikiria kabisa huyu jamaa hakuwa na mpinzani, na ikumbukwe vizuri kuwa, aliyekuwa anagombea kiti hicho cha ubunge kwa tiketi ya CCM, ambaye pia ni mbuge wa sasa wa Shinyanga Mjini, ushindi wake huwa ni wa mashaka hadi leo.

Uchaguzi wa mwaka 2010 ambapo alipita kwa tofauti ya kura anazozijua yeye na mawakala wake ilikuwa ni kitendawili kisicho na jawabu. Historia huwa na tabia ya kujirudia. Wakati huo rufaa ilikatwa na kamanda Shelembi kupinga matokeo batili na kesi iliunguruma katika mahakama ya kanda iliyoko mkoani Tabora. Hilo ndilo kosa! Kesi ilikwenda na kipindi cha mwisho kabisa, tukamkosa kipenzi chetu, hadi leo huwa sijui nini sababu ya kifo chake.

Kwa nin nimemkumbuka Kamanda Shelembi?
Ni baada ya kujirudia kwa ushindi wa ajabu tena kwa uchaguzi wa mwaka jana ambapo pia, licha ya wingu kubwa la sintofahamu juu ya Mbuge wa sasa, alishinda tena ambapo ni sintofahamu kubwa, yaani hadi mitaa alikowahi kukabwa na vijana wa mtaa nako alitwaa ushindi, ni maajabu makubwa.

Sina maana ya kumchambua Masele, ila tu kwa leo nilitaka kuwakumbusha wana wa Shinyanga kwa nia ya dhati kabisa kuwa, hebu tumuenzi kamanda Shelembi.

Nakumbuka sera zake kabambe za kutaka kukabiliana na majizi kama alivyoyaita bila uoga na kuahidi kwamba, yeye angeingia bungeni, asingenunua shangingi kama wengine wanavyofanya, ila angenunua suzuki kwa kubana matumizi kwa maendeleo ya mkoa na hata taifa. 

Tunakukumbuka kamanda Shelembi, pumzika kwa amani huko uliko, mbele yako, nyuma tupo...!

Chapisha Maoni

0 Maoni