ANGELLAH KAIRUKI: Vijana jishughulisheni na kazi zingine kuliko kusubiri ajira, maana suala la uhakiki watumishi halijulikani litaisha lini.

Dar Es Salaam
Leo kuna baadhi ya vijana waliositishiwa ajira zao walikuwa ofisi ya utumishi na utawala bora dar es salaam vijana hao ni moja ya kundi kubwa la watu 3000 walioajiriwa mwezi june 2016 na kusitishiwa ajira zao baada ya kusainishwa mikataba na kuanza kazi vijana hao leo wamefanikiwa kuonana na waziri wa utumishi wa umma Angellah Kairuki pamoja na katibu mkuu utumishi wa umma vijana walikuwa na swali moja la kuuliza kwa waziri na katibu mkuu wizara waliwauliza ni lini watarudishwa kazini ? waziri kairuki alijibu kuwa yeye hajui kuwa
ni lini watarudishwa kazini maana hata yeye anapokea maelekezo kutoka juu na kutekeleza kairuki alijibu kuwa hata yeye ofisini kwake hili zoezi analiona kero anatamani hata liishe leo ila hana jinsi kwa sababu halipo chini ya ofisi yake kwa sasa katibu mkuu aliongezea na kusema kama zoezi lingekuwa kwao walikuwa wanatamani likamilike hata leo hii viongozi hao walisema mwenye mamlaka ya zoezi hilo ni la mhe.rais hivyo na wao hawajui juu ya swala la uhakiki litaishi lini.

waziri kairuki na katibu waliomba vijana hao waliositishiwa ajira kujishughulisha na shughuli zingine kuliko kusubiri maana zoezi hilo haliratibiwi na ofisi hivyo pia vijana hao waliuliza swali la nyongeza je ajira zao zipo au zimefutwa ? waziri kairuki alisema kuwa kuna mawili wayategemee kutoka kwa mh.rais kufutwa ajira na kuanza upya au kutofutwa alisema hayo yote wayategemee kwa sababu serikali imebadilisha muundo wake hivyo taratibu za ajira mpya zaweza badilika kwa sababu serikali hii itakuwa imefanya mabadiliko.

Chapisha Maoni

0 Maoni