Je, una ndoto ambayo imefifia? Makala hii inakuhusu.

Umekwama na ndoto zako zinafifia? Makala hii inakuhusu!
Maisha yana changamoto nyingi sana ambazo kamwe huwezi kuzikwepa. Ukikubali changamoto hizo zikuzuie kufikia malengo yako uliyojiwekea, hujipendi na huna tamaa ya
kufanikiwa katika maisha yako!


Kwa nini nasema hujipendi na huna tamaa ya kutaka kufanikiwa katika maisha yako, nataka kuzungumza na wale ndugu zangu ambao wamejikuta wakikwama katika mambo yao, kufilisika na hatimaye ndoto zao za mafanikio kuyeyuka. it’s okay ni hali ya kawaida katika maisha jambo kama hilo kutokea kwani wewe sio mtu wa kwanza kutokewa na hali kama hiyo. Sasa hebu elekeza akili na mawazo yako hapa kwani naamini hutaondoka kama ulivyokuwa kabla hujasoma Makala hii. Tiba kubwa ya matatizo yanayofanana na hayo ni kukubali na kuanza upya na kukitafuta tena kilele cha mafanikio. Katika maisha kuna wakati unapitia hatua mbalimbali za mafanikio. Lakini pia, naweza ukajikuta umepoteza vitu vyote na kurudi kama zamani au Zaidi, Hayo ndio maisha. Hata kama umepoteza kila kitu umebaki na afya yako ikiwa imara, shukuru sana kwani huo ndyo mtaji pekee na ushindi mkubwa uliobaki nao. Inawezekana kuanza upya, kuanguka kibiashara siyo mwisho wa maisha, kupoteza ulichokuwa nacho siyo mwisho wa kila kitu. Tayari imeshatokea, huwezi kubadili hilo. Sawa umepata hasara, unadhani huo ndio mwisho wa maisha yako? Hapana! Maisha lazima yaendelee cha msingi hapo ni kukubaliana na matokeo na kukaa chini na kutuliza akili. Kama kuna mahala umejikwaa na kuanguka, nyanyuka haaraka na uendelee na safari. Kamwe usipaangalie mahala ulipojikwaa. Hapakuhusu tena, achana napo. Songa mbele na mapambano ya maisha. Kuwa tayari kuanza upya. Ikifika mahali huoni njia basi itengeneze mwenyewe. Pia kumbuka hutakiwi kufikiria sana historia yako ya nyuma, mafanikio hayako nyuma bali mbele unakoelekea. Achana na historia mbaya ya huko nyuma, hichi=o ulichokipoteza unaweza ukakirejesha Zaidi ya hicho, hayo ndio maisha. Kama njia ya kwanza imeshindwa kukufikisha unapotakaa kwenda, ni wajibu wako sasa kutengeneza njia nyingine. Mwanasaikologia mmoja aliwahi kusema “kwenye kutafuta mafanikio unapokosa njia, basi tengeneza njia”. Usiruhusu maisha yakuongoze/yakuendeshe, bali maisha yaongoze wewe. Mwandishi mmoja wa vitabu aitwaye Michael Gian aliwahi kupata ajali  mbaya ya ndege . akapoteza miguu yote na kupooza kuanzia shingoni hadi kiunoni! Akafilisika baada ya kuingia madeni makubwa wakati wa kutibu majeraha na afya kwa ujumla. Lakini jamaa huyo alianza upya kwa kuwatia watu moyo. Akawa anazungumza akiwa kwenye kiti cha kusukuma cha matairi. Akihamasisha watu kujikomboa na umaskini. Leo hii ni bilionea na anamiliki viwanda na ndege kadhaa kama usafiri wake binafsi. Hayo ndio maisha na mtu huyu akufanye wewe uamini kwamba, ukianguka bado unaweza kusimama na ukafanya mambo makubwa Zaidi. Yaani unaweza kupata mafanikio Zaidi hata ya uliyokuwa nayo hapo awali. Wakati mwingine Mungu humfilisi mtu kwa makusudi pengine mtu ajifunze kuishi kuanzia chini kwenda juu.


Hivyo basi huna sababu ya kujiona mnyonge na kuhisi safari yako ya kuelekea kwenye mafanikio imeishia njiani, huo uwe mwanza wa kupambana na trust me hakuna linaloshindikana ukiamua kupambana.

Chapisha Maoni

0 Maoni