Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo azindua Digital Clinic Ngorongoro.




Kwa Mara ya Kwanza Tanzania

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ndg. Mrisho Gambo amezindua Kituo cha Tiba Mtandao (Digital Clinic) kilichopo kwenye Kijiji cha Ololosokwan Wilayani Ngorongoro


Kituo ambacho Ni cha kwanza Tanzania Na kitaweza Kitoa huduma bora Na Za kisasa Kwa njia ya Mtandao Kwa wananchi zaidi ya elf kumi katika maeneo hayo ambayo hapo awali walikua wanatembea umbali mrefu zaidi ya Km 50 kufuata huduma Za Afya.

Hii inamaanisha mwananchi wa Ololosokwan anaweza kuhudumiwa Na Daktari bingwa aliyeko Muhimbili au kokote Duniani kupitia Klinik hii.

Kituo hiki kimepatikana Kwa ushirikiano Na Unesco, Samsung pamoja Na Serikali ya Tanzania.

Chapisha Maoni

0 Maoni