Waziri Jenista Mhagama kutatua kilio cha ajira kwa vijana nchini.

Waziri wa vijana sera na mipango ,walemavu Jenista Mhagama jana alikuwa mkoani Simiyu kwa ajili ya kufungua tamasha la vijana linalohusu fursa mbalimbali zinazopatikana nchini zinatumiwaje na vijana.


Waziri wa vijana alitoa ahadi kuwa atawapa ardhi vijana ili wajikite kwenye kilimo pamoja na hivyo vijana waliwasilisha kero zao zinazohusiana na ajira kusitishwa na wengine walioajiriwa mwezi May 2016 waliosimamishwa kazi na serikali huku ikiwa imewasainisha mikataba ya kazi na kuanza kufanya kazi lakini walisimamishwa bila kulipwa stahiki zao na bila kuambiwa watarudishwa lini kazini.

Vijana mkoani Simiyu na mikoa jirani walimuomba Waziri huyo jana kuokoa wimbi la hawa vijana ambao hawajui hatima yao na familia zao.

Waziri Mhangama alidai kuwa ajira ktk taifa letu ni tatizo lakini alikili kujitaidi jinsi ya uwezo wake kutatua kero zinazowakabiri vijana nchi maana vijana ni nguvu kazi ya taifa alisema.    

Chapisha Maoni

0 Maoni