IMEFAHAMIKA, KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU KULIPA 20,000 YA TCU NI KUISAIDIA SERIKALI

Kuanzia mwaka huu wa masomo,wanafunzi wa vyuo vikuu watakuwa wanalipa Tshs 20,000/ kila mwaka, ni makadirio ya Tshs bil.4 kwa wanafunzi wote, kusaidia kuendesha taasisi ya serikali inayoitwa TCU. MAHENGA BLOG imeshtushwa.


Ikumbukwe kwamba kila mwanafunzi aliepata kuomba udahili kupitia TCU alishachangia elf 50,isiyorudishika, haijalishi alipata udahili ama la.

Asilimia kubwa ya wanafunzi walioomba kujiunga na vyuo vikuu,hawakupata mikopo hiyo kwa kile kinachoitwa kukosa sifa, na tumeshuhudia baadhi ya wanafunzi hao wakilia hadharani baada ya kukosa mikopo, sasa inapotokea kwamba wanafunzi hao waliokosa mikopo wakawa ombaomba, wanapolazimishwa kulipa elf 20 kama kigezo kimoja wapo cha kudahiliwa, ni kuwaongezea wazazi wanaopigika mtaani,jukumu lingine katika safari ya watoto wao kutimiza ndoto zao za kielimu.

Chapisha Maoni

2 Maoni

  1. Blog yako imekaa vizuri mkubwa.cha kuongezea kwenye mawasiliano weka na Email yako mkuwa kuna watu watakutafuta kibiashara watashindwa.

    JibuFuta
    Majibu
    1. Dah, asante kwa ushauri kaka, sasa hivi naweka kaka, nashukuru sana na Mungu akubariki

      Futa

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA