KAGERA: Mvua ya mawe ya dakika 20 imeharibu mazao na kuengua paa za nyumba

Mvua ya mawe ya barafu iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha kwa muda wa dakika 20 imesababisha maafa makubwa kwa wananchi wa kitongoji cha Kigambo kijiji cha Kasuro wilaya ya Ngara mkoani Kagera ambapo watoto watatu wa familia moja wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na kuta za nyumba, kaya 39 kukosa makazi huku mashamba na miti mikubwa ikisombwa na maji.


Akithibitisha kutokea kwa maafa yaliyozikumba familia 39 mwenyekiti wa kijiji cha Kasuro Bw.Peter Rusesa wakati akizungumza na ITV iliyotembelea eneo hilo na kujionea hali halisi ya uhalibifu wa mashamba, nyumba kuanguka na miti mikubwa kuvunjika amesema kuwa mvua hiyo imesababisha madhara makubwa kwa jamii wakiwemo wazee.

Baadhi ya waathirika wameiambia ITV kuwa mvua hiyo imeanza kunyesha majira ya saa tisa mchana huku maeneo mengine jua likiwaka hali iliyowashangaza kwa maajabu ya kupata mvua katika kitongoji cha Kigambo na kuwasababishia janga la kukosa makazi na mashamba ya Migomba ya ndizi kuhalibika vibaya.

Chapisha Maoni

0 Maoni