KAMPALA: CHUO KIKUU CHA MAKERERE KUFUNGWA KWA MUDA USIOJULIKANA.

Idara ya polisi nchini Uganda imeamuru chuo kikuu cha Makerere kifungwe mara moja kwa muda usiojulikana. Hii ni kutokana na mgomo wa wahadhiri ambao wanaidai serikali madai yake ya ziada ambapo waliamua kuishinikiza ili kutimiza ahadi hiyo.


Akiongea kwa niaba ya serikali, waziri wa elimu, ambaye pia ni mke wa Rais, Bi. Janeth Museven amesema, wanafunzi hawafundishwi kutokana na mgomo unaoendelea wa wahadhiri.

Aidha, jeshi la polisi limewataka wanafunzi wote walioko chuoni na wale ambao wanaishi nje ya chuo hawataruhusiwa kubaki, na hata wale wanafunzi wa kimataifa wanatakiwa kusaidiwa na ubalozi wa nchi husika ili kurejea nchi kwao.

Chapisha Maoni

0 Maoni