"KAZI YA SERIKALI SI KUJENGA VIWANDA, NI KUPIGA SOUND WAWEKEZAJI WAJE WAJENGE" ASEMA MWIJAGE.

Waziri wa maendeleo ya viwanda Mhe. Charles Mwijage amesema, kazi ya serikali ni kupiga sound wawekezaji waje wajenge viwanda, na si serikali kujenga viwanda, hivyo wizara yake imejitahidi kupiga sound na viwanda sasa vinajengwa.


Ameongea hayo kwenye kipindi cha maswali na majibu alipokuwa anajibu swali la Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Godbless Lema lililoulizwa na Mhe. Khadija Ali kwa niaba yake lililomtaka kusema viwanda vitajengwa lini. "...nimepiga sound, wakaja kuwekeza..."alisema Mhe. Mwijage.

Mhe. Cecilia Pareso aliuliza swali la nyongeza kwa waziri wa viwand lililokuwa na sehemu mbili:
(a) Ni lini serikali itafufua kiwanda cha general tire."tukiangalia bajeti, serikali ilitoa bilioni 60 kwenye wizara hiyo, lakini mpaka sasa ni bilion 2 tu zilizotolewa na serikali hii iliyofilisika, ni lini kiwanda cha general tire kitafufuliwa?"
(b)Lini wafanyakazi wanaokidai kiwanda cha general tire watalipwa?

Mhe. Mwijage alimtaka Mhe.Pareso amkabidhi nakala ya madai hayo, naye ameahid kufuatilia madai hayo. Sambamba na hilo, Mhe. Mwijage aliendelea kusisitiza kuwa viwanda vinajengwa na kazi yake ni kupiga sound.

Chapisha Maoni

0 Maoni