KIMENUKA: WANANCHI SINGIDA KASKAZINI WAPINGA HUJUMA ZA MBUGE WAO NYALANDU

Wananchi wa Singida kaskazini wakiongozwa na wazee wamepinga mpango wa kuhamisha makao makuu ya wilaya ya Singida vijijini toka mji mdogo wa Ilongero na kupelekwa barabara kuu iendayo Arusha katika eneo la njia panda ya Merya, Uamuzi huo unatengua maamuzi ya Baraza la madiwani lililopita waliopitisha mji mdogo wa Ilongero kuwa unakidhi vigezo vya kuwa makao makuu ya wilaya. Tayari wananchi wameanza vikao kuunganisha nguvu zao ili kufikisha malalamiko yao ngazi za juu serikalini na Chama Cha Mapinduzi 


Mnamo tarehe 27/10/2016 baraza la madiwani wilaya ya Singida walipitisha maamuzi ya kuhamasisha makao makuu ya wilaya toka mji mdogo wa Ilongero kwenda njia panda ya Merya, Uamuzi wa Baraza la madiwani umefanyika kimizengwe bila kuwashirikisha wananchi wa Singida kaskazini.
Kuna taarifa zisizo na shaka kwamba mpango wa kupeleka makao makuu yakajengwe Porini karibu na barabara iendayo Arusha umesukwa na Mbunge Lazaro Nyalandu na hivyo ameshinikiza madiwani kupitisha kwa kura ya ndiyo. Sasa wananchi wanasema haiwezekani makao makuu ya wilaya yahamishwe kinyemela kwenda Porini kwa matakwa ya mtu mmoja anayetumia misuli ya fedha kufanya anachotaka kwa masilahi yake binafsi.
Mpango wa kuhamisha makao makuu ya wilaya ya Singida ulianza muda mrefu, Lengo ni kuhamisha makao makuu ya wilaya hiyo yaliyopo Singida mjini kwa Sasa kwenda kwenye eneo la wilaya kijiografia na ilikubaliwa na Baraza la madiwan lililopita kwamba Ujenzi wa makao makuu ya wilaya ufanyike katika mji wa ILONGERO, sehemu ambayo ndio katikati ya wilaya

Baada ya Baraza la madiwani lililopita kupitisha mji wa Ilongero kujengwa makao makuu ya wilaya Kuna maandalizi kadhaa yamekwishafanyika kama sehemu ya maandalizi ya Ujenzi wa makao makuu ya wilaya ya Singida katika mji wa Ilongero, Baadhi ya maandalizi ni pamoja na kutengwa kwa eneo la kujengwa makao makuu ya wilaya, Eneo hilo tayari liliwekewa vipimo na mipaka kwa ajili ya maandalizi ya Ujenzi wa Majengo ya Halmashauri

HOJA ZA WANANCHI WANAOPINGA HUJUMA ZA KUHAMISHA MAKAO

Wananchi wanasimamia hoja Zifuatazo :

1. NI AHADI ZA VIONGOZI WAKUU WA NCHI KUWA MAKAO MAKUU YAWE MJI MDOGO WA ILONGERO, IKIWEMO AHADI YA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE WAKATI YUKO KWNY KAMPENI MWAKA 2010 KIJIJINI ILONGERO.

2. NI AHADI YA KATIBU MKUU WA CCM ABRAHAMANI KINANA AKIWA ZIARANI SINGIDA KASKAZINI MWAKA 2015.

3. NI AHADI YA MBUNGE WA JIMBO HILI LAZARO NYALANDU AKIWA KWENYE KAMPENI ZA KUOMBA KURA MWAKA 2015.

4. KIJIJI CHA LONGERO INAKIDHI VIGEZO VYOTE VILIVYOTOLEWA TAMISEMI/SERIKALI KWA AJILI YA KUPEWA HADHI YA MAKAO MAKUU YA WILAYA. IKIWAMO;
== HUDUMA ZA AFYA
==NYUMBA /MAKAZI
== KITUO CHA POLISI
==HUDUMA ZA SOKO
===BARABARA
===ENEO KWA AJILI YA MAJENGO MBALIMBALI
=== HUDUMA ZA MAJI SAFI
===KITUO CHA POLISI.
====UMEME.

JE NI KITU GANI HASA KIPYA KILICHOJITOKEZA LEO HADI KUIKWEPA ILONGERO?

zipo taarifa zisizotia shaka kuwa madiwani walitishwa na kuhongwa ili wakubali maamuzi haya ya kijuha ya kupeleka makao makuu nyumbani kwa viongozi wakuu wa wilaya wenye ushawishi katika hili. Mbunge,mwenyekiti wa CCM wa wilaya na mweka hazina wa CCM wa wilaya ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri pamoja na katibu mwenezi wa ccm wa wilaya wote wanatokea eneo hilo. Pia wapo viongozi wengine wakubwa ndani ya serikali hii ya Magufuli wapo nyuma ya mpango huu kwa sababu wamezaliwa eneo hilo

Mgogoro huu unaweza kuzorotesha shughuli za maendeleo usipotafutiwa ufumbuzi mapema, Natoa wito kwa viongozi wa Chama na serikali kuingilia kati mgogoro huu kwa kusikiliza hoja za pande zote ili kaweka mambo sawa.

Chapisha Maoni

0 Maoni