UDAKU: ZARI, THE LADY BOSS AKOSA SALAMU YA KUZALIWA KWAKE TOKA KWA MAMA DIAMOND, BADALA YAKE ZAENDA KWA WEMA.

Mwezi wa tisa huwa ni mwezi wa sherehe kwa walimbwende maarufu hapa Bongo na hata Afrika Mashariki, yaani Zari Hassan, Wema Sepetu na Vera Sidika. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, walimbwende hawa wote wamezaliwa mwezi wa tisa kwa siku tofautitofauti, yaani tarehe 23 kwa Zari, 28 kwa Wema na tarehe 30 kwa Vera.



Tarehe 23 ya mwezi wa tisa, Zari alifikisha umri wa miaka 36, na sherehe kubwa ilifanyika Zanzibar na Diamond kuoneka kufanya kufuru ya kumpa zawadi ya nyumba yenye thamani ya shilingi milion 18 za Kenya mlimbwende wake. Kilichokuja kushangaza, mama yake Diamond, Bi. Sandra Kassim hakumpa zawadi yoyote, wala hakumtumia ujumbe wowote wa kumtakia siku njema ya kuzaliwa. MAHENGA BLOG ikashtushwa na kuamua kufuatilia...

Siku tano baadaye, @kendrah-michaels (Sandrah Kassim) kama anavyofahamika kwenye mtandao wa Instagram alinukuliwa na blog yetu akimtakia siku njema ya kuzaliwa mlimbwende Wema Sepetu, mpenzi wa Diamond wa zamani, kitendo ambacho kimeonekana kumuumiza kwa THE LADY BOSS. Hawa ndiyo mastaa wetu wa nyumbani.

Chapisha Maoni

0 Maoni