Wimbi
la utupaji watoto wachanga wenye umri wa siku moja hadi kumi na mbili
kwenye maeneo ya karibu na hospitali, mitaroni jalalani na kando ya
vituo vya kulelea yatima limezidi kushika kasi katika mkoani wa Arusha
ambapo kwa kipindi kifupi inadaiwa zaidi ya watoto themanini
wameokotwa na wasamaria wema na kupelekwa kwenye vituo vya kulelea
watoto .
Katika uchunguzi uliofanywa kwenye baadhi ya vituo vya kulelea watoto
wenye mazingira magumu umegundua idadi hiyo ni kwa vituo viwili tu vya
Samaritani na Faraja ambako wasamaria wema waliookota watoto
waliwapeleka akiwemo mtoto wa siku kumi na mbili anayedaiwa kuokotwa
hivi karibuni pembezoni mwa hospitali ya Seliani huko Ngaramtoni huku
walezi wa vituo hivyo wakidai wamekuwa wakishirikana na jeshi la polisi
pamoja na maafisa ustawi wa jamii wanapofikishiwa watoto wanaookotwa.
Wakizungumzia matukio hayo baadhi ya wasamaria wema wamesema tabia hiyo
inatakiwa kukomeshwa kwani kitendo hicho kinawanyima watoto haki ya
kuishi na kuwataka watanzania kuwa na tabia ya kuwasaidia watoto hao
wasiyo na hatia.
Baadhi ya watoto waliyotelekezwa na kuokotwa na wasamari wema miaka ya
nyuma ambao hivi sasa wamekuwa na kumaliza elimu ya msingi wameeleza
kitendo hicho kinavyo waumiza na kuwataka watanzania kuwaona kwa jicho
la huruma.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA